We start with a song, I am sure you know it "Kiswahili kitukuzwe...kwani lugha ya taifa, baba mama na vijana tutukuzeni Kiswahili"
Hehehe If your Swahili reading skills are wanting, I suggest you look away or look for an interpreter right about now..here goes..
Hamjambo dungu na dada zangu, karibuni nyote kwenye makala haya ya mipira yenye umbo isiyoeleweka, natumai wiki hii imekua yenye heri na fanaka kwenu kama ilivyokua kwangu. Basi bila kupoteza wakati, wikendi nyingine ya Raga imewadia, kwanza tutazame ratiba ya mechi zitakazo andaliwa kwenye daraja mbali mbali, kuanzia ligi kuu yaani Kikombe cha Kenya (hehehe), ngao ya Eric Shirley hadi ligi za kitaifa Mashariki na Magharibi.
Ligi Kuu.
Machine Vs Kisumu (UoN)
Homeboyz Vs Quins (RFUEA )
Strathmore Vs KCB (Ruaraka)
Nondies Vs Impala (Jamuhuri )
Nakuru Vs Mwamba (Nakuru Athletic Club)
Ngao ya Eric Shirley.
Machine II vs Western Bulls
Homeboyz II vs Quins II
Strathmore II vs KCB II
Nondies II vs Impala II
Nakuru II vs Mwamba II
Ligi ya Kitaifa Magharibi.
Moi Univesity vs Kisumu II
Kisii vs Masinde Muliro
Bungoma vs Maseno
Eldoret vs Webuye
Siaya vs Kakamega
Ligi ya Kitaifa Mashariki.
Mombasa Poly vs USIU
Pwani Uni vs Spartans
JKUAT vs Mombasa
KCA vs Blakblad
Ligi ya Vyuo Vikuu.
Nazarene vs Blakblad II
Daystar vs Catholic
Egerton vs Kenya poly.
Comras vs Thika
Kabarak vs KEMU
Baada ya michezo iliyokua wiki iliyopita, ifuatayo ni jedwali ya ligi kuu, nitaorodesha timu na alama ilizonazo. Kwa ligi zinazofuata mtani wia radhi kwani sijapata takwimu hizo mpaka wa sasa :
LIGI KUU.
- KCB – 34
- Nakuru –33
- Strathmore - 33
- Mwamba - 30
- Quins - 30
- Impala- 27
- Nondies – 17
- Machine - 15
- Kisumu - 12
- Homeboyz – 10
Nitafanya hima kupata takwimu hizo haraka iwezekanavyo, haya basi tutazame mechi zinazotarajiwa jumamosi hii.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi yaani Machine wana wa alika vijana kutoka kondele yaani Kisumu katika uga wao wa Nairobi. Wanafunzi hao watakua wakitarajia kulipiza kisasi, kwani waliposafiri kisumu kwenye mkondo wa kwanza wa ligi, walikungutwa kwa alama 32-5. Duru za kuaminika ziliniarifu wakati huo ya kwamba vijana wa eschuma hawakusafiri wote kwenda Kisumu na ndio ilikua sababu yao kuu ya kushindwa. Roundi hii hawatakua na sababu yoyote iwapo watashindwa tena. Timu ya Kisumu itatarajia kuwahakikishia kwamba ushindi huo haukua wa kibahati, mechi hii itakua ngumu kwa pande zote mbili ijapokua Machine wameonyesha mchezo mzuri kwenye mechi zilizopita (ukitoa ile dhidi ya Quins juma lililopita) na basi watakua na uhakika fulani wa kushinda.
Timu ya Quins ita ialika timu ya vijana wa santuri yaani Homeboyz katika uga wa RFUEA, vijana hao wa nyumbani waliwa adhibu Quins kwenye mkondo wa kwanza 12-5. Na watataka kuwahakikishia Quins ya kwamba ushindi huo haukua wa kismati kwa kurudia ushindi wao. Quins nao ambao wameinua mchezo wao kwa kadri kutoka mechi hiyo watataka sana kulipiza kisasi kwani kichapo hicho bado kinawanyima usingizi wengi wao. Vijana wa santuri ambao wako kwenye nafasi ya mwisho watanuia kujikwamua kutoka kwenye nanga iliyowafungia humo. Quins nao wanakaribia kilele cha ligi na hawatataka kuzuiwa na yeyote, natarajia mechi hii iwe ya kukata na shoka.
Timu ya Nondies ita ikaribisha jirani wake wa karibu Impala kwenye uwanja wa jamuhuri. Itakumbukwa wawili hawa walipopatana hapo awali kwenye uga wa Impala, vijana wa Impala waliweza kuwapiku wageni wao kwa alama 22-12 kwenye dakika za mwisho wa mechi hiyo. Mara hii Nondies watakua na motisha mara dufu kwani wali ishinda Mwamba wikendi iliyopita na watataka kuwika kwenye uwanja wao wa nyumbani. Impala nao pia walipata ushindi wikendi iliyopita, ushindi huo dhidi ya Strathmore vile vile utawapa motisha vijana hao wanaovalia jezi za nyekundu. Mechi hii kama ile ya mkondo wa kwanza itakua ngumu kwa pande zote mbili na ni alama chache sana ambazo zitawatenganisha wawili hawa.
Timu ya Mwamba hali maarufu Kulabu, watasafiri hadi Nakuru kukabiliana na timu ijulikanayo kwa jina la utani, Wanyore. Mara ya mwisho wawili hawa kumenyana, kulabu ilipata ushindi japo mdogo, wa alama 18-15. Nakuru wako kwenye nafasi ya pili, alama tatu mbele ya Mwamba walio kwenye nafasi ya nne, kwa hivyo tarajia mechi ya kusisimua watakapo ingia uwanjani. Wanyore hawajashindwa kwenye uga wao wa Nakuru Athletic Club msimu huu na hawata tarajia kuanza wikendi hii, Mwamba nao walijipata kwenye nafasi ya nne baada ya kushindwa na Nondies na watataka kupanda hatua kadhaa baada ya mechi hii. Nikichungulia kwenye darubini yangu ya unabii, naona ya kwamba mechi hii itakua ngumu zaidi kuliko ile ya kwanza, ina uwezekano wa kuisha kwa alama sawa ama kwa ushindi wa alama mbili au moja.
Namalizia na mechi ambayo natarajia itachezwa kwenye uga wa Ruaraka, ambapo vijana wa chuo kikuu cha Strathmore watakua wageni wa KCB. Timu hiyo ya benki imo kileleni mwa ligi, baada ya kuishinda Homeboyz kwa alama 6-3, Strathmore nao wako kwenye nafasi ya tatu baada ya kushindwa na Impala kama nilivyotaja hapo awali. Wawili hawa walipopatana mara ya mwisho kwenye uwanja huu huu, KCB wali ibuka washindi kwa alama 14-10.Vijana wa kikosi cha ishirini na saba watakua wakinuia kugeuza matokeo hayo na kurudi kwenye kilele cha ligi. Ilhali KCB watakua na ari ya kuyarudia matokeo hayo na kumaliza mechi wakiwa kifua mbele ili waendelee kukita kambi katika nafasi ya kwanza ya ligi. Mechi hii ndio nitakayo hudhuria na kuichambua siku ya Jumatatu. Hii ni mechi nyingine ambayo itakua ya kumezea mate, na ya kukata na msumeno wacha shoka!
Kwa taanzia, michuano ya Super Rugby yaling'oa nanga asubuhi hii, ambapo timu ya Crusaders iliponea chupu chupu dhidi ya Blues kwa alama 19-18, mechi zingine zita chezwa hii leo na hapo kesho, kama hujui ni mechi zipi mpaka sasa hivi, huwezi saidika. Mechi za Nchi sita pia zitaendelea..
Kufikia hapo naomba niwa age kwaheri, na niwatakie wikendi iliyobubujikwa na raha na starehe popote pale mtakapo kua. Nitachambua michuano ya Bamburi kwa kina wiki ijayo, kwa hayo na mengine mengi tu…tuonanane wakati huo..
Na Kwa hayo mabibi na mabwana……….
KWISHA!!!!
Ni mimi wenu, Kijana Mtanashati….
Poghie.
waaah c nmetake tym kusoma.......swa c ni ngumu gai!!!
ReplyDeleteYet eti ulipitia shule! hehehe
DeleteHongera kaka,
ReplyDeletethis must have taken u ages to compile.
Good work pitseh.
jim
Close to two weeks, na unajua swa doesn't have spell checks!
DeleteNingependa kukosea matumishi ya tamthilia na maana fiche katika misamiati mbali mbali ambayo umetumia kuuandika mseto huyu wa mwanaspoti wa mchezo wa raga.
ReplyDeleteTembelea maktaba tafadhali.
Mimi wako
mwenzangu...inaonekana unayo chinda ya matamchi!!!kwani siyo kukosea ni kukosoa na siyo mseto huyu ila ni nseto huu...asante! hehehe
DeleteMimi napendekeza umuone mwalimu mati..Lakini kwa haya machache ambayo umeweza kuyaandika kwa muda wa wiki moja pongezi!!!!
Delete***Hamjambo dungu*** hapo naona kweri kwaba una chida ya matamuchi....good work though
ReplyDeleteHahahaha waaahhh, yenyewe hapo siwezi jitete! thanks man..
Deleteumeandika makala mazuri sana.Asante ndugu. Ishirini na saba
ReplyDeleteKiswahili kitukuzwe!
ReplyDeletei got losted!!!!! nitatumia the thorax approach kuelewa
ReplyDeleteHahahaha...kwenda!
DeletePlease note, the Nondies vs Impala game will be played at St. Mary's School. Strathmore vs KCB will be at the Impala grounds.
ReplyDeleteEnjoy.